2017-01-17 14:32:00

Watoto wahamiaji wanapofika Ulaya wanakumbana na changamoto kubwa


Katika tukio la kila mwaka kwa siku ya Kimataifa ya Wahamiaji  na Wakimbizi , Carita ya Ulaya unaungana mkono Baba Mtakatifu Francisko katika wito wa kila mtu kuwa makini kwa hali halisi ya wahamiaji watoto, hasa ambao Baba Mtakatifu Francisko anasema “wako peke yao na waathirika mara tatu, kwanza  wao ni watoto, pili ni wageni na tatu hawana wa kuwalinda na kuwatetea.Tunawaomba nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya , kuzingatia kikamilifu, maslahi bora ya watoto na katika kujibu kesi za watoto hawa wasio kuwa wazazi wao,na pia wanaotafuta ulinzi”. 


Caritas inatoa baadhi ya ushuhuda kwa mfano wa mtoto wa miaka 8 na 15 kutoka  nchi ya Afghanstan  waliokuwa wanaomba msaada kutokana na vikosi vya kigaidi Isis  kuteka nyara ndugu zao,na wao kutembea kwa miguu kwa mwezi mmoja na nusu kufika nchini Ugiriki na kwa bahati mbaya  walipoteza wazazi wao  na hawajuhi mahali walipo licha ya hiyo wandai kwamba ili kutoka Uturuki kufika Ugiriki walilipa kiasi cha Euro 1,000 kila mmoja.
Ujumbe unasema kwamba maslahi ya mtoto imeelezwa katika  mkataba wa Umoja wa Mataifa wa haki za Mtoto ukisema, “matendo yote yanayo husu watoto, yawe yaliyofanywa  na taasisi ya Umma au binafsi kwa ustawi wa jamii, mahakama za sheria, mamlaka tawala  au bunge; kwamba  maslahi hayo lazima ya zingatie ubora  wa misingi hiyo. Misingi hiyo ndiyo pia  inaelezwa katika katiba wa Haki na Msingi kwenye  Umoja wa nchi za  Ulaya.Kanuni hii ni muhimu kweli katika kesi za watoto wadogo.Mahitaji yao maalumu lazima yawekwe kipaumbele zaidi kabla ya kuzingatia mengineyo. Zaidi ya hayo yote watunga sheria , wanasiasa, na shughuli nyingine  lazima kujali suala hili na kuhakikisha kwamba ulinzi wa watoto hao unapata ufanisi wa haraka iwezekanavyo.


Halikadhalika Caritas ya Ulaya inasema ,wahamiaji kimataifa ni suala ambalo huathiri mamilioni ya watoto, kwani Takwimu kulingana na makadirio ya UNICEF , inasema karibu milioni 50 ya wahamiaji wamekuwa wakiingia kwa kwa kasi zaidi na zaidi ya nusu yao milioni 28 wamekimbia makazi yao kutokana na vita na vurugu.
Akiongeza zaidi  Katibu Mkuu wa Caritas  wa Ulaya Bwana  Jorge Nuno Mayer alisema: Ni watoto wengi wasio na wazazi wao , na wahamiaji wengi wanao lazima kuhama makazi yao kwa matumaini ya kupata usalama  na amani.Lakini kwa upande wa watoto ,wanapofika nchi za Ulaya wanakabiliwa na uhaba wa usalama na mapokezi, ambapo vifaa vya wafanyakazi havitoshelezi au  kuridhisha, wakati mwingine havikuandaliwa  na pia ukosefu wa mafunzo  ya kukabiliana na mahitaji yao.Kwa hali hiyo ni kweli watoto wanafanya uzoefu wa kutisha juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Baada ya safari nzito wakiwa hawana ndugu au wazazi wao , wanakosa mwongozo ulinzi, faraja na kujikuta katika mazingira mageni na magumu.

 

Licha ya hayo ni watoto wanakabililiana na  matatizo makubwa zaidi kuliko watu wazima katika kukabiliana na mahitaji kwa mfano  urasimu na taratibu za kutambuliwa.Alimazia akisema Kwa kuzingatia changamoto hizi nyingi, Caritas ya Ulaya  inataka kuunga mkono wito wa baba Mtakatifu Francisko juu ya kuwatunza watoto , kuwatetea wahamiaji ambao hawana njia za kulindwa na kuomba makazi. Katika kujibu zaidi maslahi bora ya watoto ni lazima viongozi wa Ulaya: kuwezesha njia za kisheria ili watoto wasitegemee walanguzi kufika Ulaya bali mataifa hayo yafanye kila iwezekanavyo katika kufanikisha zaidi makazi mapya na malengo ya kibinadamu ya uandikishaji;vilevile kwa Kuzingatia juu ya kuwaunganisha na familia zao , ndugu ikiwezekana au kuwakabidhi katika familia nyingine ili kuhakikisha kuwa watoto wahamiaji wasio na wazazi wanapata familia,wanapewa nafasi ya kuishi maisha yao  kwa ukamilifu ndani ya usalama wa familia hizo.Halikadhalika wakikishe wanawatafutia visa watu wanao lazimika kukimbia nchi zao kwa kutafuta ulinzi na usalama katika nchi nyingine.Na mwisho kuimarisha ulinzi ikiwa  ni lazima kuwatafutia ulinzi wakati wa kufiri salama na kulipa fedha za kusafiri kwa kawaida badala ya wakimbizi hao kutumia fedha zao kwa walanguzi.

 

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatica

 








All the contents on this site are copyrighted ©.