Kwenye somo la liturjia ya siku kutoka katika kitabu cha Wahebrania ,ni mambo
matatu ya kutazama katika kuishi maisha ya kikristo kwa kutazama wakati ulio pita
, uliopo na ujao. Na zaidi tunaitwa kufanya kumbukumbu, kwasababu maisha ya kikristo
hayakuanza leo , bali yanaelendelea . Kufanya kukmbukumbu ni kukumbuka kila kitu kwa
yale mambo mema na yale yasiyo mema , na kutengenza historia , mbele ya Mungu bila
kuifunika na kuificha.
Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Misa Takatifu Ijumaa 27 Januari 2017
katika Kikanisa cha Mtakatifu martha Mjini vatican, akisema ndugu zangu tufanye kumbukumbu
za wakati ule wa mwanzo, kwani ni siku za furaha , za kuendelea mbele katika imani
na hasa unapoanza kuishi kwa imani, nakatika mateso ya majaribu. Huwezi kutambua
maisha ya kikristo ,maisha ya kila siku ya kiroho bila kuwa na kumbukumbu.
Anasisitiza na siyo tu kutotambua , bali huwezi kuishi maisha ya kikristo bila kuwa
na kumbukumbu ya ukombozi wa Mungu katika maisha yangu, kumbukumbu ya majanga yangu
ya maisha , na ni jinsi gani Mungu ameniepusha na majanga hayo.Kumbukumbu ni neema
, ya kuomba ili Bwana aweze kusahau yaliyopita , na hata mimi pia ni sisahau kipindi
kile kizuri au kibaya ; furaha na mateso ya misalaba . kwa njia hiyo mkristo ni mtu
wa kumbukumbu.
Anaendelea kufafanua akisema ,Mwandishi wa barua hiyo anatufanya tuelewe kwamba sisi
sote tuko safari ya matarajio ya jambo flani, ambapo itafikia kikomo cha kukutana
,yaani kukutana na Bwana,anatuhimiza tushi kwa imani.Matumaini utazama wakati endelevu
, kwa njia hiyo haiwezekani mkristo kuishi bila kuwa na kumbukumbu za mambo yaliyotendeka
, haiwezekani mkriso kuishi maisha yake bila kutazama wakati endelevu kwa matumaini
ya kukutana na Bwana.
Baba Mtakatifu anasisitiza kwamba Yeye anasema sentensi nzuri ya kwamba “ Bado muda
kidogo , na hivyo Maisha ni kama upepo maana yanapita.Anatoa mfano kwamba mtu akiwa
kijana ufikiria bado anao muda mrefu , lakini maisha tanatufundisha japokuwa ni maneno
yasemwayo na kila mmoja ya kwamba tazama muda ulivyo pita! namjua tangu utoto na sasa
anaoa! Hama kweli muda unapita kwa haraka.Lakini matumaini ya kukutana na Bwana ni
mvutano kati ya kumbukumbu na matumaini , wakati uliopita na endelevu.
Hali kadhalika barua inatualika kuishi wakati uliopo ,japokuwa mara nyingi kuna
machungu na mateso ,ujasiiri na uvumilivu: yaani, tunapaswa kusema ukweli, bila aibu,
kuvumiliana katika maisha : sisi ni wadhambi Baba Mtakatifu anasisitiza aliye wa
kwanza na hatakayekuja baadaye , maana hatuwezi kufanya orodha , kwasababu wote tu
wadhambi.Wote tunakwenda mbele kwa ujasiri na uvumilivu . Sio kubaki tumesimama kwani
kusimama hakutuwezeshi kukua.
Hatimaye mwandishi wa Waebrania natuhimiza tusitende dhambi , ambayo huzuia kuwa
na kumbukumu, matumaini, ujasiri na uvumilivu.Woga ni dhambi inayokuzuia usiende
mbele kutokana na hofu uliyo nayo wakati Yesu anatueleza “ msiogope “walio na hofu
mara nyingi ubaki nyuma kwa kufunga wao wenyewe kuotokana na woga huo.
Usije hatarisha tafadhali, Baba Mataktafi anasema bali uwe na taadhali, kwani kuna
matumaini kwa kila mtu , usiache ugandizwa na ukasahau hata neema nyingi ulizopokea
.Hofuinakuondolea matumaini ya kuendelea mbele .Mkristo unapaswa kuishi wakati uliopo
na tayari bali usiwe na sawa na mtu anapokuwa njiani , mvua ikaanza kunyesha wakati
nguo aliyo vaa siyo nzuri ikajikunyata yote na kumbana, hiyo inaelezea juu ya mioyo
yenye kujikunyata yenyewe , iliyo na woga kwani hiyo ni dhambi dhidi ya kumbukumbu
, ujasiri, uvumilivu na matumaini.Bwana atusaidie kukuza kumbukumbu , matumaini ,
na atupatie kila siku ujasiri na uvumilivu, atuondolee ule woga unao tufanya tuwe
na hofu ya kila kitu , mioyo iliyo fungwa , migumu wakati Yesu mwenyewe anasema anaye
hifadhi maisha yake mwenyewe atapoteza.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |