Wito wa Maakofu wa Marekani kwa ajili ya kutetea heshima ya utu wa binadamu umetolewa
kutokana na kukosoa hatua iliyotolewa na Rais mpyaTrump kutokupokea wakimbizi ndani
ya nchi yake.Tendo hilo limekuwa tayari ni joto binafsi la maaskofu wa Kamati ya Baraza
la Maaskofu wa Marekani anayeshughulia idara ya wakimbizi Askofu Joe Steve Vasquez
wa Jimbo la Austin aliye waeleza Viongozi wa Baraza la maaskofu wa Marekani wakati
wa kikao chao.
Taarifa ya saini ya rais na makamu wake , Kardinali Daniel N.na di Nardo Askofu Mkuu
wa Galveston –Houston, Askofu Mkuu José Horacio Gómez wa Jimbo kuu la Los Angeles
,wanatoa wito kwa waamini wote katoliki wawe na sauti moja , kwaajili ya kutetea heshima
ya utu wa binadamu.Kwa upande wa maaskofu siyo kwamba wanaingilia moja kwa moja maandamano
ya kisiasa ya umma,bali ni kukumbuka Injili isemayo kwamba kumpokea mgeni ni miongoni
mwa utume wa maisha ya mkristo.
Akitoa mfano kutoka katika kipengele cha Mtaguso wa Pili wa Vatican,hasa katika
tamko la “nyakati zetu”(notra aetate) maaskofu wanabainisha msingi wa nguvu ya upendo
na haki isiyo kuwa na mwisho ambayo ndiyo uhusiano uliopo kati ya Wakristo na Waislam.
Wakisikistizia kuwa Kanisa, halitakosa kamwe kutetea ndugu wote wa madhehebu yanayo
kabiliwa na mateso na unyanyasaji mikononi mwa watesi wao.
Kwa maana hii, wanakumbusha kwamba wale ambao hukimbia kutoka katika serikali ya
Kiislam na katika vikosi vingine vyenye msimamo mkali wanajitoa sadaka ya kila kitu
hata kile chenye thamani katika miliki yao kwa jina la mani na uhuru." Hawa ni watu
binafsi na familia ambao wanatafuta usalama kwa watoto wao.
Kwa njia hiyo maaskofu wanatoa wito juu ya mapokezi. Bila shaka ni lazima kuwa macho kuhusu hatari ya uwezekano wa kuingiliwa na vikundi vya kigaidi katika taifa, lakini wanapaswa kuwakaribisha na kuwaona kama wao ni washiriki wa kupambana na maovu yote.Wanasema kwamaba Kwani mahali ambapo hakuna mapokezi ya watu,ni bayana vitendo vya ubaguzi na kutelekezwa kutokea, na hivyo maaskofu wanasema wao watakuwa sauti kwa niaba yao.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |