Vatican itatoa mchango mkubwa kwa kuchangia shughuli zinazoendelea za ukarabati wa Kanisa la Kaburi Takatifu Yerusalem na Kanisa Kuu alipozaliwa Bwana wetu Yesu Bethlehemu . Hayo yamethibitishwa na Issa Amil Kassissieh Balozi mwakilishi wa nchi ya Palestina nchini Vatican katika Shirika la Habari la Fides. Nia ya Vatican kufanya hivyo pia ilimethibitishwa kwenye ofisi za ubalozi na Kardinali Leonardo Sandri , Rais wa Baraza la Kipapa kwa Makanisa ya nchi za Mashariki , kwenye mkutano wao uliofanyika tarehe 27 Februari 2017 mjini Vatican.
Chini ya usimamizi wa Ndugu wadogo wa Mtakatifu Francisko wa Assisi , wanaotunza
maeneo matakatifu huko Yerusalem,Balozi anasema watawatangazia ni kiasi gani cha mchango
na utaratibu upi utumike kuwafikia kiasi hicho, anaongeza; kwa sasa, kwa niaba ya
Rais wa nchi ya Palestina , Mahmud Abbas na watu wote wa Palestina ninatoa shukrani
kwa Vatican katika juhudi zao kuendelea kusimamia katika kuleta haki na mani kwa nchi
Takatifu,ambayo ni maeneo aliyozaliwa na kusulibiwa Bwana wetu Yesu kristo.
Ukarabati wa Kanisa kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo huko Bethlehemu ulianza
mwaka 2013, unaoshirikisha Jumuiya tatu za kidini ambazo ni Jumuiya ya Waorthodox
wa kigiriki, Waarmenia na Wafranciskani ambao ndiyo wapo ni wasimamizi wa Kanisa Ku
una hawa,ndiyo wenye haki na usimamizi wa mali ya Kanisa kwa mujibu wa katiba ya
Status Quo.
Kwa upande wa kazi ya ukarabati wa Maktaba ya Kanisa la kaburi Takatifu ulianza Mei 8 2016.Pamoja na hayo Mpango wa ukarabati wa Kanisa la kaburi Takatifu unatakiwa gharamia dola milioni 3.3 ambazo zitatolewa kwa ushirikiano kutoka Kanisa la Orthodox wa Kigiriki, Kanisa la Waarmenia na Kanisa Katoliki.Mwezi Aprili 2016 Mfalme wa Joardan Abdallah II alitoa mchango wake binafsi kwa ajili ya mpango huo na Oktoba mwaka jana Rais Mahmoud Abbas wa Palestina naye pia alitoa mchango binafsi kusaidia ukarabati wa maktaba ya Kanisa la Kaburi Takatifu.Ndugu wadogo wa Mtakatifu Francisko ambao ni walinzi wa maeneo matakatifu kwa kupitia njia zake za mawasiliano, mara kwa mara wanatoa taarifa rasmi juu ya maendeleo ya kazi inayoendelea.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |